tunakuchimbulia mpaka mwisho

Ajira ni ngumu

No comments
Daressalaam, shirika la mapato tanzania (TRA) hapo jana liliitisha mchakato wa kufanyisha watu interview kwa ajili ya kuwapatia ajira watu kadhaa,katika ukumbi wa Diamond .

Takribani watu elfu tano walihudhuria interiew hiyo, hii inaonyesha jinsi gani sakata la ajira lilivyo gumu nchini. Inasemekana kuna baadhi ya watu walipangiwa kufanya interview asubuhi, lakini mpaka inafika mida ya saa saba, hakukua na utaratibu unaoeleweka kitu ambacho kilifanya watu wengi kuondoka eneo hilo la kufanyia interview na kukata tamaa kurudi hapo.
Inasemekana ilivyofika mida ya saa nane mchana hivi ndo uongozi wa TRA wakaanza kuita watu, takribani watu watatu walikua wanaitwa kwa awamu moja, sasa embu fikiria hao watu zaidi ya elfu mbili wataweza kufanyishwa interview kwa speed ya watu watatu kwa awamu, ni kazi sana.
Sakata la ukosefu wa ajira.
Tanzania ni nchi inayojitahidi kwenye kuendelea, lakini kuna baadhi ya vitu naweza sema serikaki yetu inavifanya labda kwa lengo la kusaidia wananchi lakini bila kujua kwamba wanaua maendeleo ya nchi.
Mfano wa kwanini hivi: hivi nyuma kidogo serikali ilruhusu sukari nyingi iingie nchini na iuzwe kwa bei ya chini ili wananchi wapate unafuu wa kuzinunua sukari hizo.
Sawa ni jambo zuri sana na la kufurahisha kwenye akili za watanzania, lakini, nchini tanzania kuna viwanda vinavyozalisha sukari, navyo vinategemea soko la wananchi wa tanzania , sasa kama wananchi wamepata sukari nyingine tena za bei rahisi, unafukiri watataka kununua hizi za nchini ambazo bei zipo juu kiasi?, haiwezekani, sasa hii ni nini kitaifa, ni kwamba , serikali kwa kufanya hivyo maana yake, wanataka kuviua viwanda vya sukari vya hapa nchini, na kama viwanda vikifa unafikiri ni nani atakayeumia, wawekezaji wa hivyo viwanda wenyewe wataondoka tu na kurudi makwao, lakini walewakulima ndo watao kufa njaaa na kurudishwa nyuma kimaendeleo, na miji mingi itakufa na kuingia kwenye umasikini.
Kwa mfano huo wa juu, wazo ambalo naona serikali ingetakiwa kufanya, ingefanya hivi: ingeziipia sukari zinazozalishwa humu ndani asilimia fulani ili bei itakayoenda kuwafikia wananchi iwe ya chini kidogo, hivyo kufanya wananchi waweze kununua sukari, na sio kuua viwanda.
Sio viwanda vya sukari tu, viko vingi ambavyo watu  wanashuhudia vinakufa, sasa kama viwanda vinakufa unategemea ajira itoke wapi, ni kazi sana.
Ningewashauri tu vijana wenzangu, watafuta ajira, waanze kuangalia upande mwingine wa ajira, kujiajiri wenyewe, watafute biashara za kufanya ili waweze kuendelea kuishi vizuri na kuukimbia umasikini.

No comments :

Post a Comment