tunakuchimbulia mpaka mwisho

WANUSURIKA KIFO BAADA YA GARI LA MIZIGO KUPARAMIA NYUMBA WAKATI WAKIWA WAMELALA,MANISPAA YA TABORA!!

No comments

Watu zaidi ya 8 wamenusurika kifo wakati wakiwa wamelala nyumbani mwao mtaa wa heri manispaa ya tabora, baada ya gari la mizigo aina ISUZU kuparamia nyumba yao, lilipomshinda dereva alipokuwa akikata kona, ambapo mama mjazito aliyenusurika amekimbizwa hospitalini akiwa na hali mbaya kutokan a na mshituko na hali yake ya ujauzito. 
Wakizungumza na ITV wananchi na mashuhuda wa ajali hiyo walioharibiwa thamani zao mbali mbali 


wamesema kuwa, umefika wakati serikali kubadili adhabu za madreva wazembe ambao wanaendesha vyombo vya usafiri bila kuzingatia sheria zilizowekwa na serikali huku wakipoteza maisha ya wananchi na mali zao. 
Akizungumza na ITV juu ya ajali hiyo na kubaini uzembe wa dereva wa gari hilo lenye namba za usajili t 396 AGS, ambaye hakupatikana mara moja, kamanda wa polisi mkoani tabora kamishina msaidizi Suzani Kaganda aliyefika eneo la ajali hiyo amesema kuwa, mwendesha gari hilo atatafutwa na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake. 
Aidha mmiliki wa nyumba hiyo bw.Ramadhani Musa Kaswezi, anayeishi kijijini ilolangulu hakusema lolote akidai kikao cha familia kitatoa maamuzi ili kuelezea hatua atakazochukua kutokana na wapangaji wake wawili kubolewa nyumba. 
CHANZO: ITV

No comments :

Post a Comment