Kaka mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Nicholaus kwa
kushirikiana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers,
amesimamia fumanizi la dada’ke ambaye ni denti wa sekondari moja jijini
Dar (majina yanahifadhiwa kwa sababu maalum) ambapo alimfumania chumbani
na njemba mmoja sharobaro aliyetajwa kwa jina la Abuu Ally, mkazi wa
Mbagala-Charambe, Dar.
Njemba sharobaro, Abuu Ally akiwa na denti baada ya fumanizi.
OFM ikiwa kazini, ilipokea malalamiko kutoka kwa Nicholaus aliyedai
kwamba amekuwa akiumizwa na taarifa kwamba kila ikifika saa 2: 00 usiku
kuna mwanaume amekuwa akijipenyeza na kuingia chumbani kulala na mdogo
wake wa kike kisha kuchomoka alfajiri.
Kaka mtu wa denti huyo akimwajibisha Sharobaro(mwenye boksa).
Nicholaus alisema kuwa mara nyingi vitendo hivyo hufanyika wikiendi
ambapo katika kuhangaika kumnasa anayemharibu mdogo wake aliwataarifu
OFM ambao waliingia mzigoni na kuweka mtego uliomnasa sharobaro huyo.
Sharo yaani Abuu Ally akijikomiti kulipa faini kwa kosa la kulala na dada wa mtu.
OFM hawakuwa wenyewe kwani walimtaarifu Mjumbe wa Mtaa wa
Maji-Matitu, Hawa Ally kuwa wana kazi eneo lake hivyo akatoa ushirikiano
uliofanikisha kumnasa Abuu.
Ama kweli za mwizi arobaini! Saa 5:11 usiku, jamaa huyo aliingia chumbani kwa denti huyo na kuanza makeke yake akimfanyia binti huyo mavituzi.
Ama kweli za mwizi arobaini! Saa 5:11 usiku, jamaa huyo aliingia chumbani kwa denti huyo na kuanza makeke yake akimfanyia binti huyo mavituzi.
Waraka wa kujikomiti wa Sharo alioundika mbele ya mjumbe, Hawa Ally.
OFM walisubiri kwa muda wa robo saa kisha wakaingia ndani ya nyumba
hiyo kwa msaada wa wapangaji na kumnasua binti huyo ili aendelee na
masomo.Sharobaro huyo alikiri kuingia mara kadhaa ndani humo na
kubanjuka na denti huyo.
Baada ya kukiri kosa mbele ya kiongozi huyo wa serikali za mtaa,
pande zote zilikubali kusuluhishwa ambapo Abuu alikubali kulipa faini ya
shilingi laki moja na kupewa muda wa siku moja kutekeleza adhabu hiyo.
No comments :
Post a Comment