Akizungumza
na Uwazi nyumbani kwa mwajiri wake aliyejulikana kwa jina moja la
Ghati, Yombo jijini Dar, Rehema aliyefika jijini hapa Januari, 2013
akitokea nyumbani kwao, Masasi mkoani Mtwara, alikuwa na haya ya
kusema:
“Nakumbuka
siku hiyo ilikuwa ni Jumapili ya Novemba 30, saa moja usiku nikiwa nje
ya nyumba ya bosi wangu. Akatokea msichana mmoja aitwaye Fatuma na
mwenzake aitwaye Ashura huku wakiwa wamebeba kisu na wembe. Wakanikamata
kwa nguvu na kunikaba, wakaniangusha chini na kuanza kunichanachana
mwili mzima.
“Wakati
huo nilikuwa naelekea nyumbani kwa akina Fatuma kuchukua sanduku langu
ambalo alilichukua kwa bosi wangu akidai kwamba nimempotezea ‘memori
kadi’ ya simu yake hivyo alisema kwamba mpaka nitakapomrudishia ndipo
nitakapochukua sanduku langu.
“Walinijeruhi
sana na kukimbia, nikarudi ndani lakini bosi wangu hakuwepo nyumbani na
aliporudi alinichukua na kunipeleka polisi, tukapewa kibali cha
matibabu (PF3) na kwenda Hospitali ya Amana kutibiwa. Tulirudi nyumbani
na baadaye tukafuatilia kesi yetu polisi, wakasema turudi nyumbani
tukaelewane mbele ya mjumbe ili kesi imalizike.
“Tulienda
kwa mjumbe pamoja na Fatuma na wazazi wake na mimi nilikuwa na bosi
wangu, wakataka kesi imalizike yaani tusameheane lakini kwa upande wa
wazazi wangu waliopo Masasi, nilipowapa taarifa walikataa kumaliza kesi
kienyeji na kutaka ifike mahakamani kwa vile watuhumiwa walikuja na
silaha na walidhamiria kuniua,” alisema Rehema.
Kwa
upande wa mtuhumiwa, Fatuma Zuberi (17), alipoulizwa na waandishi wetu,
alidai kwamba wakiwa njiani na mdogo wake wakienda dukani kununua
vocha, walivamiwa na Rehema na kushambuliwa akitaka wamrudishie sanduku
lake.
Naye
mama mzazi wa Fatuma aliyejitambulisha kwa jina la Sharifa Mwinyi
Kondo, alidai kwamba mwanaye pia amejeruhiwa hivyo waliamua mambo yote
yaishe kwa kusameheana mbele ya mjumbe wao. Mjumbe wa shina namba 22,
Rose Kiravu alipoulizwa kuhusu ishu hiyo alikiri kupokea taarifa hizo na
kudai kwamba suala hilo lilifika polisi lakini lilirudishwa kwake kwa
upatanishi ambapo alikaa na pande zote mbili pia wajumbe wa nyumba kumi
wawili na wote waliamua kusameheana.
No comments :
Post a Comment